Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 46 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 600 2023-06-12

Name

Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga minara ya simu katika Kata za Masisiwe, Udwekwa na Nyanzwa Wilayani Kilolo?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Justin Lazaro Nyamoga, Mbunge wa Jimbo la Kilolo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ilibaini changamoto ya upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika Kata za Udekwa, Nyanzwa na Masisiwe ambapo tayari imekwishawapata watoa huduma wa kufikisha huduma za mawasiliano katika kata za Masisiwe na Nyanzwa wakati Kata ya Udekwa itaingizwa katika orodha ya miradi itakayotekelezwa kulingana na upatikanaji wa fedha, ahsante.