Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 49 | Natural Resources and Tourism | Wizara ya Maliasili na Utalii | 650 | 2023-06-15 |
Name
Emmanuel Peter Cherehani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ushetu
Primary Question
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza:-
Je, lini Serikali itamaliza mgogoro wa mpaka wa Pori la Usumbwa Forest Reserve na Hifadhi ya Pori la Kigosi Moyowosi – Ushetu?
Name
Mohamed Omary Mchengerwa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Rufiji
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA K.n.y. WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Emmanuel Peter Cherehani, Mbunge wa Ushetu, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Pori la Usumbwa Forest Reserve ambalo kwa sasa ni Hifadhi ya Taifa Kigosi, haina mgogoro wowote wa mpaka na wananchi wa Ushetu. Kwa sasa kilichopo, wananchi wa Ushetu waliwasilisha maombi ya kumegewa eneo ambapo Serikali inaendelea na tathmini na pindi itakapokamilika, wananchi watajulishwa, nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved