Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 50 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 653 2023-06-19

Name

Leah Jeremiah Komanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Meatu

Primary Question

MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza:-

Je, Serikali haioni haja ya kuigawa Shule ya Msingi Mwanhuzi kwa kuwa shule hiyo ina wanafunzi 1,400?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Leah Jeremiah Komanya, Mbunge wa Jimbo la Meatu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli Shule ya Msingi Mwanhuzi ina changamoto ya mlundikano wa wanafunzi. Katika kutatua changamoto hiyo katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 Serikali kupitia Mradi wa BOOST imepeleka shilingi milioni 348.5 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya katika Kata ya Mwanhuzi. Baada ya kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo, changamoto hii itakuwa imetatuliwa.