Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 52 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 690 | 2023-06-21 |
Name
Abubakar Damian Asenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilombero
Primary Question
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanzisha Tawi la Chuo Kikuu Huria katika Halmashauri ya Ifakara?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Abubakari Damian Asenga, Mbunge wa Kilombero, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Serikali haina mkakati wa kuanzisha Tawi la Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania katika Halmashauri ya Ifakara. Aidha, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kimefungua matawi yake katika Makao Makuu ya Mikoa yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo Mkoa wa Morogoro ambapo wananchi wa Halmashauri ya Ifakara wanapata huduma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania pia kina vituo vya mitihani kwenye ngazi ya wilaya kwa pale ambapo idadi ya wanachuo ni 50 na kuendelea. Nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved