Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 57 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 761 2023-06-28

Name

Tunza Issa Malapo

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TUNZA I. MALAPO aliuliza:-

Je, ni wanafunzi wangapi wamerejea shuleni tangu waraka wa kuwaruhusu utolewe?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia napenda kujibu swali la Mheshimiwa Tunza Issa Malapo, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mpaka kufikia mwezi Januari, 2023 wanafunzi waliorejea shuleni kuendelea na masomo ya elimu ya sekondari ni 1,907 ambapo waliorudi katika mfumo rasmi ni 562 na waliorejea nje ya mfumo rasmi wa elimu kupitia Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) ni 1,345.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa wanafunzi wa elimu ya msingi; Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais - TAMISEMI inaendelea kukusanya taarifa za wanafunzi waliorejea shuleni baada ya kukatiza masomo kwa sababu mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, ninakushukuru.