Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 53 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 695 2023-06-22

Name

Yahya Ally Mhata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itafanya ukarabati katika Kituo cha Afya cha Nanyumbu?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ally Yahya Mhata, Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na uchambuzi na mapitio ya vituo chakavu vinavyohitaji ukarabati katika ngazi ya afya ya msingi ili bajeti ya Serikali ikiruhusu vituo hivyo chakavu viweze kufanyiwa ukarabati kikiwepo Kituo cha Afya cha Nanyumbu.