Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 53 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 703 2023-06-22

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. GRACE V. TENDEGA K.n.y. MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwapatia msaada wa kisaikolojia watu waliopitia ukatili wa kijinsia?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Cecilia Daniel Paresso, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imeanzisha vituo 22 vya huduma ya mkono kwa mkono (One Stop Centres) kwa ajili ya hospitali za mikoa 13 ikiwemo Dar es Salaam, Pwani, Mbeya, Iringa, Kilimanjaro, Shinyanga, Mwanza, Arusha, Tabora, Morogoro, Kigoma, Dodoma na Simiyu kwa ajili ya kuwahudumia waathirika wa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Vituo hivyo hutoa huduma za kipolisi, ushauri nasaha na huduma za afya. Lengo la Serikali ni kuwa na kituo angalau kimoja kwa kila Mkoa. Vilevile kuna nyumba salama 11 nchini na Madawati ya Jinsia katika vituo vyote vya polisi na magereza. Ahsante.