Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 25 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 217 2022-05-18

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya ya Makete?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKAO NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Festo Richard Sanga, Mbunge wa Jimbo la Makete, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali katika mwaka wa fedha 2022/2023 imeitenga shilingi milioni 900 kwa ajili ya kufanya ujenzi na ukarabati wa majengo ya Hospitali hiyo ili iweze kuwa na miundombinu bora yenye hadhi ya Hospitali ya Wilaya, ahsante.