Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 27 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 237 2022-05-20

Name

Janejelly Ntate James

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANEJELLY J. NTATE aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itapeleka Askari Polisi katika Kituo cha Polisi Kata ya Kilungule - Mbagala ili wananchi wa kata hiyo wapate huduma?

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Janejelly James Ntate, Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Dar es Salaam, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali tayari ilishakipangia askari sita kituo kidogo cha Polisi cha Kata ya Kilungule - Mbagala na kinafanya kazi saa 24. (Makofi)