Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 29 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 248 2022-05-24

Name

Miraji Jumanne Mtaturu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Mashariki

Primary Question

MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itamaliza changamoto ya kuchelewesha mafao kwa wastaafu?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu, Mbunge wa Singida Mashariki, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imefanya jitihada mbalimbali za kulipa Deni la Mfuko wa PSSSF ikiwa ni pamoja na kutoa Hatifungani ya Shilingi Trilioni 2.17 ambazo zitaimarisha mtiririko wa mapato na kuwezesha kutoa mafao kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuanzia Julai Mosi, 2021 hadi Tarehe 30 Aprili, 2022, wastaafu na wanufaika 24,757 wa Mfuko wa NSSF wamelipwa jumla ya Shilingi Bilioni 78 na wanufaika 42,427 wa Mfuko wa PSSSF wamelipwa jumla ya Shilingi Trilioni 1.99. Serikali inawahakikishia wastaafu wote nchini kwamba, itaendelea kuwalipa mafao yao kwa wakati.