Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 45 Justice and Constitutional Affairs Wizara ya Katiba na Sheria 399 2022-06-16

Name

Kavejuru Eliadory Felix

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buhigwe

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itajenga Mahakama ya Wilaya ya Buhigwe ili wananchi waweze kupata huduma?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kavejuru Eliadory Felix, Mbunge wa Buhigwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Buhigwe ni moja kati ya miradi ya Mahakama inayotekelezwa katika mwaka wa fedha 2021/2022. Kupitia programu ya maboresho ya Mahakama, Mkandarasi wa ujenzi wa Mahakama hii amepatikana ambaye ni Lucas Construction na kukabidhiwa eneo la ujenzi mwezi Oktoba, 2021. Kazi za ujenzi zinaendelea na zinatarajiwa kukamilika ifikapo Julai, 2022.