Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 32 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 275 2022-05-27

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais ya ujenzi wa soko la kisasa la Kwa Sadala?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Saashisha Elinikyo Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Hai imeandaa andiko la mradi wa ujenzi wa soko la Kwa Sadala wenye thamani ya shilingi bilioni tisa. Andiko hilo limefanyiwa uchambuzi na Mkoa ambapo mapungufu yaliyojitokeza yamewasilishwa Halmashauri kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho.

Mheshimiwa Naibu Spika, pindi marekebisho hayo, yatakapokamilika na kukidhi vigezo Serikali itatafuta fedha kutoka vyanzo mbalimbali kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.