Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. John Danielson Pallangyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Mashariki
Primary Question
MHE. DOROTHY G. KILAVE K.n.y MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza: - Je, ni lini Serikali itatoa kiasi cha fedha ilizoahidi kwa ajili ya matengenezo ya barabara ya Malula Kibaoni hadi Ngerenanyuki?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii niweze kuuliza swali la nyongeza. Nashukuru pia Serikali ya Chama cha Mapinduzi chini Mama yetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutupa fedha Shilingi Bilioni Moja mwaka jana ambazo ndizo zimetumika kutengeneza barabara hii kwa kiwango cha changarawe.
Mheshimiwa Spika, swali, barabara hii ni moja ya ahadi ya Mheshimiwa Rais ili ijengwe kwa kiwango cha lami. Je, Serikali inasemaje kuhusu hilo, ni lini itajengwa kwa kiwango cha lami?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. John Danielson Pallangyo, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, hatua ya awali ni hii ambayo tunarekebisha hii barabara ili walau iweze kupitika kipindi chote wakati ambapo tunatafuta fedha kwa ajili ya kutekeleza hiyo ahadi ya kujenga kwa kiwango cha lami. Kwa hiyo, nimhakikishie tu kwamba Serikali ya Chama cha Mapinduzi ambayo inaongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan itatekeleza ahadi yake kwa vitendo. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved