Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Alfred James Kimea
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Korogwe Mjini
Primary Question
MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga miundombinu ya umwagiliaji katika mabonde ya mpunga ya Kwamgumi na Kwamsisi - Korogwe?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii kuuliza swali la nyongeza. Pia napenda kuipongeza Serikali kwa majibu yake mazuri na yenye kutia matumaini kwa wananchi wa Kata ya Kwamsisi pamoja na Kwamngumi kwa kuwa hiki kilikuwa kilio chetu sisi sote.
Mheshimiwa Spika, swali langu la nyongeza, ninahitaji commitment ya Serikali kwamba ni kweli mwaka huu tutaenda kujengewa Skimu hii ya Kwamsisi na mwakani tutaenda kujengewan Skimu ya Kwamngumi maana imekuwa ahadi ya siku nyingi. Kwa hiyo, naomba commitment ya Serikali kwamba jambo hili linaenda kutokea mwaka huu na mwaka ujao.
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kama ambavyo nimejibu katika jibu la msingi, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini, ahadi ya Serikali tulivyoahidi hapa itatekelezeka kwa asilimia mia moja. Hiki ninachokizungumza, nina uhakika nacho, ahsante sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved