Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Joseph Kizito Mhagama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Madaba

Primary Question

MHE. JOSEPH K. MHAGAMA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kutengeneza barabara ya Wino hadi Ifinga ambayo wakati wa masika haipitiki?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH K. MHAGAMA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kupata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, barabara hii kwa kipindi cha miaka mitatu imetumia zaidi ya Bilioni Moja kuijenga na Serikali imeashaweza kutoa fedha hizo, hii ni dhahiri kwamba Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la barabara hii. Haa hivyo, barabara hii bado kuna kipande cha kilomita 18 kutoka Ifinga Mjini kuelekea Kitongoji cha Muungano na Ruhuji kilometa 18.

Je, ni lini sasa Serikali itaifungua barabara hii kuelekea eneo hilo la Ruhuji?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Joseph Kizito Mhagama, Mbunge wa Jimbo la Madaba, kama ifutavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali inafanyakazi kubwa na kwa kuwa Mheshimiwa Mbunge ameomba ongezeko la eneo la barabara la kilomita 18 kutoka Ifinga kwenda kwenye Kitongoji cha Muungano, basi naawagiza TARURA Mkoa wa Ruvuma pamoja na Halmashauri ya Madaba waende wakapitie barabara hiyo na wafanye tathmini na baada ya hapo watuletee fedha ili tuweze kui-extend. Ahsante sana.