Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Sophia Hebron Mwakagenda
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itakuwa tayari kuongeza bei ya chai Wilayani Rungwe kutoka shilingi 340 hadi shilingi 700 kwa kilo hasa ikizingatiwa kupanda kwa gharama za mbolea na madawa?
Supplementary Question 1
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Mheshimiwa Waziri suala la bei ya chai tumekuwa tukilisemea kwa muda mrefu sana ni kweli katika jibu lako la msingi mnasema kuna mnada wa chai kule Mombasa. Sisi kama Taifa tunajitosheleza kwa chai ya Rungwe, chai ya Njombe na kule Lushoto kwa nini msiweke mnada katika Taifa letu kwa sababu tunao wateja wa kutosha? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Umehamasisha Wawekezaji kuwekeza katika chai lakini wapo wawekezaji ambao hawaendi sawa na wakulima maeneo ya Rungwe kwa kutokuwapa pesa zao kwa wakati lakini tu si hivyo wanajiita Wakulima Estate lakini wakulima kama wakulima wahausiki ni mradi wa mtu binafsi. Serikali mtachukua hatua gani kuhakikisha jina hilo litumike sawa sawa na wakulima wanavyohitajika? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nimpongeze Mheshimiwa Mwakagenda kwa kufuatilia suala hilo la chai na kama tulivyojibu katika jibu letu la msingi, kwamba mkakati wa sasa wa Serikali ni kuhakikisha tunakuwa na mnada ndani ya nchi na kama alivyoainisha yale maeneo yote kwamba tuna maeneo mengi na chai inatosheleza na huo mkakati na ndiyo njia pekee ambayo itatusaidia kuongeza bei na kuimarisha soko la ndani la chai. Kwa hiyo, tumelipokea na tunalifanyia kazi na tutapata majibu haraka iwezekanavyo.
Mheshimiwa Spika, hukusu hawa wawekezaji ambao hawaendi sawa na Wakulima nitoe tu rai kwamba sisi kama Wizara tutakwenda tutakaa nao ili kuhakikisha kwamba hizi changamoto ambazo zinajitokeza haziendelei tena, ahsante sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved