Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Charles John Mwijage

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba Kaskazini

Primary Question

MHE. CHARLES J. MWIJAGE aliuliza: - Je, ni lini Serikali itapeleka Fibre Speed Boat mbili zilizofunikwa kama ambulance ili kusaidia Wananchi wa Visiwa 39 vya Wilaya ya Muleba?

Supplementary Question 1

MHE. CHARLES JOHN P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nisikitike kwa majibu ya Serikali. Serikali imegawa ambulance lakini sisi Wilaya ya Muleba ambayo 70% ni maji na kuna visiwa 38 hatuna kifaa sio dharura yaani ndiyo maisha yetu visiwa 38 vinahitaji vesal realiable vesal ya ku-move. Serikali hamuoni kwamba mchukue jitihada za Mheshimiwa Rais ku-copy ile vesal mliyopeleka Mafia na sisi mtununulie kama hiyo kusudi wananchi waweze kufika katika sehemu za huduma kwa sababu eneo hilo lina watu wengi.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba tu nimuhakikishie Mheshimiwa Mwijage kwamba Serikali ya awamu ya Sita inatia kipaumbele cha hali ya juu sana katika maeneo ambayo hayafikiki kuhakikisha kwamba huduma za rufaa zinatekelezwa ipasavyo. Ndiyo maana sasa imeandaa mpango makakati wa kuainisha maeneo yote ambayo ni magumu kufikika yale ambayo yanahitaji boat ambulance ikiwemo Halmashauri ya Muleba.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishie kwamba tayari tupo hatua nzuri na mwaka ujao wa Fedha 2024/2025 tunaanza kutenga fedha kwa ajili ya kupata hizo boat ambulance.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.