Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Selemani Moshi Kakoso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpanda Vijijini
Primary Question
MHE. MOSHI S. KAKOSO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa fedha za kujenga mabweni katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Bulamata?
Supplementary Question 1
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Halmashauri ya Wilaya ilishatenga shilingi milioni 50 na wananchi wamejitolea kwa nguvu zao, wamefyatua tofali takriban milioni moja kwa kata nzima.
Je, Serikali imejipanga vipi kuwasaidia, kuwaunga mkono ili waweze kukamilisha mabweni hayo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; Shule ya Bulamata watoto wanaosoma wanasoma takriban kilometa tano mpaka zaidi ya kilometa tano kuifikia shule hiyo.
Je, Mheshimiwa Waziri haoni kwamba ni wakati muafaka wa kuwasaidia hawa vijana kupeleka fedha na kuwasaidia gari ambalo litakuwepo pale kwenye hiyo shule ili liweze kusaidia huduma kwenye emeo la shule?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali madogo ya nyongeza ya Mheshimiwa Moshi Selemani Kakoso, Mbunge wa Mpanda Vijijini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kuwaunga mkono wananchi katika jimbo lake, ni kwamba jambo hilo Serikali tunalifanya. Moja katika hatia ya kwanza ni tuliwaagiza Halmashauri kutenga fedha za ndani, lakini na sisi, nimuahidi tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, tutatafuta fedha kwenye vyanzo vingine ili tuweze kuongeza na kuwasaidia wananchi hao ambao wamejitahidi kwenye ujenzi wa shule.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hilo ni sawasawa tu na swali lake la pili la msingi, kwamba tutatafuta fedha ili tuweze kuongeza na kumalizia shule yao na hayo mabweni, ili sasa watoto waanze kusoma kutokana na umbali huo. Ahsante sana.
Name
Minza Simon Mjika
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MOSHI S. KAKOSO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa fedha za kujenga mabweni katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Bulamata?
Supplementary Question 2
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kuuliza swali; je, ni lini Serikali itajenga mabweni katika Shule ya Kimali Sekondari, Wilayani Meatu?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mwenyekiti, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Minza Mjika, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatafuta fedha, na kwa sababu tuna miradi mingi katika Idara ya Elimu basi tutalipa kipaumbele katika fedha ambazo zinakuja kutoka kwenye wafadhili mbalimbali, ahsante sana.
Name
Michael Constantino Mwakamo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kibaha Vijijini
Primary Question
MHE. MOSHI S. KAKOSO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa fedha za kujenga mabweni katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Bulamata?
Supplementary Question 3
MHE. MICHAEL C. MWAKAMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pale Jimboni Kibaha kwenye Kata ya Kwara na Magindu kuna mabweni mawili-mawili kila shule ya sekondari yaliyojengwa kuanzia mwaka 2018 hadi 2019 ambayo hayajakamilika na mabweni haya yangekamilika yangewasaidia watoto wanaotokea katika Kijiji cha Dutumi na Kijiji cha Lukenge ambao ni umbali wa karibu kilometa kumi kila kimoja.
Je, Serikali ina mpango gani wa kutuongezea fedha ili kukamilisha majengo yale ili watoto wayatumie?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mwakamo, Mbunge wa Kibaha Vijijini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, katika bajeti yetu tumetenga fedha kwa ajili ya kumalizia baadhi ya mabweni ambayo yalijengwa katika EP4R Awamu ya Saba na Awamu ya Nane ambayo yalikuwa katika mwaka 2017/2018 katika bajeti kuu, kuhakikisha tunamalizia ili mabweni yale yaanze kutumika yakiwemo ya jimboni kwake. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved