Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Primary Question
MHE. DANIEL B. SILLO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itamaliza migogoro ya mipaka kati ya Vijiji vya Vilima Vitatu, Mwada na Ngolee dhidi ya Hifadhi ya Tarangire?
Supplementary Question 1
MHE. DANIEL B. SILLO: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; kwa kuwa migogoro hii husababishwa na wahifadhi kutokushirikisha viongozi au wananchi wa maeneo husika wakati wanapoongeza mipaka hii ya hifadhi.
Je, Serikali haioni ni muhimu sana kuwashirikisha viongozi na wananchi wa maeneo husika, ili kupunguza igogoro hii ambayo imedumu kwa muda mrefu?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; je, Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari kufanya ziara katika jimbo langu, hasa maeneo haya yenye migogoro ya mipaka na vijiji vyetu na kufanya mkutano mikutano ya hadhara, ili wananchi waeleze na ikiwa ni sehemu ya utatuzi wa migogoro hii? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Mary Francis Masanja
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyomgeza ya Mheshimiwa Daniel Baran Sillo, Mbunge wa Babati Vijijini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ni kweli kumekuwa na changamoto hii ya namna ya kutafsiri mipaka na imesababisha wananchi kutoidhishwa na utatuzi huu. Nimuahidi Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Babati Vijijini kwamba tutafika na kuwashirikisha wananchi kutatua na kutafsiri mipaka ya eneo hili.
Mheshimiwa Spika, swali lingine ni utayari wa Wizara, akiwemo Waziri; tuko tayari kwenda kutoa ufafanuzi, lakini pia na kuzungumza na wananchi, ahsante.
Name
Francis Kumba Ndulane
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kaskazini
Primary Question
MHE. DANIEL B. SILLO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itamaliza migogoro ya mipaka kati ya Vijiji vya Vilima Vitatu, Mwada na Ngolee dhidi ya Hifadhi ya Tarangire?
Supplementary Question 2
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali langu ni kwamba, je, ni lini Serikali itamaliza migogoro kati ya wanavijiji wa vijiji vya Nakingombe, Mtepela pamoja na Zinga Kibaoni dhidi ya Pori la Akiba la Selous katika Wilaya ya Kilwa?
Name
Mary Francis Masanja
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Francis Ndulane, Mbunge wa Kilwa, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ni kweli mgogoro huu tunautambua na niliwahi kufanya ziara katika maeneo hayo. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tutafika kutatua mgogoro huu ikiwemo kutoa ufafanuzi kwa wananchi, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved