Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Tarimba Gulam Abbas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kinondoni
Primary Question
MHE. TARIMBA G. ABBAS aliuliza: - Je, nini kauli ya Serikali juu ya Bima za Afya kwa watoto?
Supplementary Question 1
MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Spika, kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, la kwanza; tunafahamu kwamba Taifa hili miaka yote limekuwa na haja ya kuhakikisha tunajenga taifa bora la kesho. Katika kujenga taifa bora la kesho maana yake ni kwamba watoto wetu wawe na afya bora kutokana na uwepo wa mfumo mzuri.
Je, Serikali haioni umuhimu wa kuwa na mfumo ambao utasaidiawa wetu kuendelea kutunzwa afya zao badala ya kukaa na kusubiri mpaka Bima ya Afya kwa Wote iweze ikaanza kufanya kazi? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili. Kwa kutokuwa na mfumo sahihi kwa ajili ya watoto na afya zao.
Je, hatuoni kwamba tunafifisha, tunapunguza hali ya taifa hili kujenga vizuri watoto wetu kwa minajiri wa kuwa citizen bora wa taifa la kesho? (Makofi)
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba kuna mifumo. Kuna mifumo tena mizuri, ndiyo maana jana umemuona Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekwenda pale Benjamin Mkapa na umeona watoto ambao ni masikini kabisa, wasingeweza kulipa zaidi ya milioni 50 ambazo zilihitajika kwa ajili ya kutibu sickle cell wametibiwa bure na wamepona. Mpaka mwaka huu, watoto zaidi ya 20 Mheshimiwa Rais wetu ametoa fedha na watarudi kwenye familia zao.
Mheshimiwa Spika, kwenye nchi hii kuna watoto milioni 31. Milioni 1.5 wako kwenye mfumo wa bima wa sasa, milioni 30.7 wako kwenye mifumo mingine, kwa maana wanatibiwa kwenye mifumo mingine iliyoko kwenye nchi yetu. Nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwamba kuna mifumo haikosi changamoto lakini hizo changamoto mimi na wewe tunavyoendelea kukabiliana nazo, kwa sababu zinatokea kila wakati. Tukikubaliana wote kwa pamoja twende kwenye issue ya Bima ya Afya kwa Wote, na hizi changamoto ndogo ndogo tunazokutana nazo leo, tutakwenda kutatua kwa pamoja Mheshimiwa Mbunge.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved