Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Salim Alaudin Hasham
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ulanga
Primary Question
MHE. SALIM A. HASHAM aliuliza:- Je, lini serikali itajenga skimu za umwagiliaji katika Jimbo la Ulanga?
Supplementary Question 1
MHE. SALIM A. HASHAM: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, Serikali imeliongezea Bonde la Mto Kilombero kwa maslahi mapana ya Taifa letu, kwa hiyo wananchi wa maeneo hayo wamekosa maeneo kwa ajili ya kilimo.
Je, ni lini Serikali itaenda kujenga mradi mkubwa, ili kutoa fursa kwa wananchi wa Jimbo la Ulanga, hususan kwenye Kata za Kichangani, Milola na Minepa, ili kupata sehemu ya uhakika ya uzalishaji mali?
Swali la pili, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya kuboresha na kuuendeleza Mradi wa Skimu ya Umwagiliaji ya Minepa yenye ukubwa wa zaidi ya hekta 1,800 ili kutoa fursa kwa wananchi wa vijiji hivyo kupata sehemu kubwa ya uzalishaji mali? Ahsante.
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwanza kama nilivyojibu katika swali langu la msingi kwamba, Skimu ya Minepa tunafanya upembuzi yakinifu na tunajua umuhimu wa skimu hiyo kwa sababu ina hekta karibu 1,800. Kwa hiyo, wakishamaliza watu wetu sisi jukumu letu ni kutafuta fedha na tutaanza ujenzi mara moja kwa sababu ya umuhimu huo.
Mheshimiwa Spika, kwa sababu hii ya kwenye swali lake la kwanza vilevile alipouliza kuhusu eneo la Bonde la Kilombero na zile Kata za Kichangani, Milola na Minepa, wananchi bado wanauhitaji. Kwa hiyo, sisi bado tuko huko tunafanya upembuzi yakinifu, tukishakamilisha tu tutatoa taarifa hata kwa Mbunge mwenyewe na Wilaya yake, lvilevile tutatafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo, ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved