Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Deodatus Philip Mwanyika
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Njombe Mjini
Primary Question
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itatatua tatizo la usafiri kwa ajili ya kusafirisha mahabusu na wafungwa katika magereza nchini?
Supplementary Question 1
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Spika, Haki ya Tume Jinai ilibainisha changamoto kubwa sana kwa Jeshi la Magereza kwa kuwa na magari chakavu sana ambayo yamenunuliwa muda mrefu sana na bajeti inayotengwa ni ndogo na hatuna uhakika kama inawafikia. Sasa nina maswali mawili.
Swali la kwanza; je, katika fedha ambazo anasema zilitengwa kwa bajeti liyopita za milioni 882 za kununua magari matano, je, yamenunuliwa na yamekwenda gereza gani?
Swali la pili; kwa kuwa, wafungwa hao Serikali inatumia gharama kubwa sana ku-maintain magari chakavu na hakuna economic benefit inayoipata mwisho wa siku. Kwa nini, Serikali isitafute utaratibu rafiki zaidi kama kuwa na mikataba ya muda mrefu kwa gharama nafuu ya kukodisha magari ambayo ni decent kwa ajili ya Watanzania hawa ambao wamejikuta kwenye changamoto kwa wakati huo? (Makofi)
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mwanyika, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, juu ya milioni 878 ninakiri kwamba fedha hizi zilichelewa kutoka lakini tunashukuru Wizara ya Fedha iliridhia ku-double kiwango hicho ndiyo maana katika bajeti ya mwaka huu 1,930,000,000 zimewekwa kwa ajili ya kununulia magari hayo.
Mheshimiwa Spika, sasa hivi mchakato wa manunuzi umeendelea na maombi ya fedha hizi Wizara ya Fedha yamefanyika ili fedha zitakapopatikana malipo yaweze kufanyika na hatimaye tuweze kupata magari husika.
Mheshimiwa Spika, kuhusu kuingia mkataba wa muda mrefu ili kuboresha haki ya wafungwa kupata usafiri, tunachukua ushauri huo ili tuweze kuufanyia kazi kuona kufanya leasing ili ikiwezekana wakati wowote wafungwa wasikwame kwenda magerezani kwa sababu ya ukosefu wa magari, nashukuru. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved