Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Rehema Juma Migilla
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ulyankulu
Primary Question
MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza: - Je, bei ya mfuko wa mbolea itakuwa shilingi ngapi baada ya Serikali kuweka ruzuku nchi nzima?
Supplementary Question 1
MHE. REHEMA J. MIGILLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyojibu Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba kwa msimu wa 2022/2023 kwamba mbolea zote ziliwekewa ruzuku, lakini napenda nimwambie kwamba mbolea ya tumbaku NPK haikuwekewa ruzuku na bei yake ilikuwa ina-range kwa dola shilingi 75. Hizi mbolea nyingine zilikuwa zinauzwa kwa nusu ya bei kutoka laki na ishirini mpaka elfu sabini mpaka elfu sitini; na hii mbolea ya ruzuku ya tumbaku kwa mwaka huo NPK imewekewa ruzuku kidogo na mbaya zaidi mbolea hii...
MWENYEKITI: Uliza swali Mheshimiwa Rehema.
MHE. REHEMA J. MIGILLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo naenda huko. Mbolea hii haiuzwi madukani bali inakopeshwa kwa wananchi wetu. Sasa swali langu, ni kwa nini mbolea hii ya tumbaku NPK haiuzwi bali inakopeshwa kwa wananchi wetu na haipo wazi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; kumekuwa kuna malalamiko mengi sana kutoka kwa wakulima wetu kwamba mbolea wanayotumia kuweka kwenye mazao yao inakuwa haina nguvu hali inayosababisha mazao yao kuwa yana udumavu na yasiyokuwa bora, katika kuthibitisha hili Mkuu wetu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Batilda Burian juzi amekamata Kampuni ya YARA ambayo ni wasambazaji na wauzaji wa hii mbolea wakiwa wanauza mbolea iliyokwisha muda wake yaani mbolea fake na wanabadilisha vifungashio.
Je, Serikali mna mpango gani wa kuhakikisha mnawasaidia hawa wananchi wote ambao wameuziwa mbolea ya tumbaku na mazao mengine, mbolea fake hali inayosababisha hao wananchi wapate mazao yasio bora? Mna mpango gani wa kuwasaidia hao wananchi? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, natambua concern ya Mheshimiwa Mbunge hususan katika mbolea ya NPK katika zao la tumbaku na kwenye tumbaku utaratibu wake ni tofauti na ruzuku inapita katika vyama vya ushirika ambavyo vyama vile ndiyo huwa vinakopesha wakulima wake na wakulima hulipa baada ya muda wa msimu. Mwaka huu baada ya malalamiko makubwa ambayo yalitokea mwaka wa fedha uliopita kwamba walikosa ruzuku, mwaka huu Serikali iliongeza ruzuku kwa kiwango kidogo na jambo hili tutalipitia upya ili kuona namna gani tutaongeza ruzuku zaidi kuwanufaisha wakulima wa tumbaku nchini. Kwa hiyo, hicho ni kitu ambacho mimi mweyewe nakifahamu na nilifika katika maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge anaelezea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Kampuni ya YARA kuuza mbolea iliyopita muda wake, mamlaka ya mbolea Tanzania (TFRA) ndiyo wenye jukumu la uthibiti na usimamizi wa mbolea nchini na kuna hatua wameshaanza kuzichukua ikiwemo kuitaka Kampuni YARA kutoa maelezo na baada ya hapo tutatoa taarifa kamili ya hatua ambazo sisi tutakuwa tumezichukuwa. Kwa hiyo, jambo hili na lenyewe lipo ofisini kwetu na tunalifanyia kazi.
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Primary Question
MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza: - Je, bei ya mfuko wa mbolea itakuwa shilingi ngapi baada ya Serikali kuweka ruzuku nchi nzima?
Supplementary Question 2
MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na msimu huu unaoendeleao wa kilimo na kipindi hiki wakulima haswa wa Mkoa wa Rukwa wanategemea sana mbolea aina ya Urea katika kukuzia mazao yao lakini upatikanaji wa mbolea hii aina ya Urea umekuwa ni changamoto kubwa hapa nchini. Nataka kusikia kauli ya Serikali ni nini juu suala la uhaba wa mbolea ya Urea?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na tunakiri kwamba baada ya Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuanzisha utaratibu wa ruzuku ya mbolea kwa wakulima matumizi ya mbolea yamekuwa makubwa kwa wananchi. Ni kweli sasa hivi kidogo mbolea ya Urea imekuwa pungufu, si kwa Mkoa wa Rukwa peke yake hata tumepata malalamiko kutoka Ruvuma kwamba wananchi wanahitaji na changamoto ilikuwa tu ni baadhi ya meli kuchelewa kufika bandarini kwa ajili ya kushusha. Kwa hiyo, kuna baadhi ambazo zipo zinaendelea kushushwa ili tuweze kuwafikishia wananchi wamalize katika msimu wao kwa sababu mbolea ya Urea inatumika kwa ajili ya kukuzia mazao.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved