Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Gibson Blasius Meiseyeki
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Arumeru-Magharibi
Primary Question
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kurasimisha na kurahisisha ubadilishaji wa fedha za kigeni kati ya Tanzania, Zambia, Malawi na Msumbiji?
Supplementary Question 1
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri naomba kuuliza swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiopingika kwamba ukienda kwenye maduka ya kubadilisha fedha za kigeni mara nyingi utakuta sarafu ambazo zimeandikwa ni za baadhi ya nchi kama Ugandan shilling, Kenyan shilling, lakini sina uhakika kama ukienda kwenye zile mbao za kubadilisha fedha utakuta kwamba imeandikwa exchange kati ya pesa ya Malawi Kwacha, Zambian Kwacha na nchi kama Mozambique. Je, kutokana na hali ilivyo ya ukosefu wa dola na jinsi pressure ilivyo kwa sasa hivi, Serikali zetu hazioni kwamba ni wakati muafaka ma-governor wa nchi hizi hasa ambazo tunapakana wakakaa ili waje na utaratibu ambao tutaweza kutumia sarafu za kwetu kupunguza pressure ya hizo dola?
Name
Gibson Blasius Meiseyeki
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Arumeru-Magharibi
Answer
WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, wazo la Mheshimiwa Mbunge makini kabisa wa Kalambo ni la msingi. Tutawaelekeza ma-governor wakae waendelee kuangalia hizi njia mbadala ambazo zinaweza zikafanyika, hasa katika nchi zinazofanya biashara mpakani ili kuweza kurahisisha biashara na kupunguza tatizo la uhitaji wa dola.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved