Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dennis Lazaro Londo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mikumi

Primary Question

MHE. DENNIS L. LONDO K.n.y. MHE. PROF. PALAMAGAMBA J. A. M. KABUDI aliuliza: - Je, lini Serikali itaandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi wa Jimbo la Kilosa kutokana na uwepo wa migogoro ya muda mrefu ya Wakulima na Wafugaji?

Supplementary Question 1

MHE. DENNIS L. LONDO: Mheshimiwa Spika, naomba kuuliza Serikali kwamba, miji midogo ambayo inachipukia kwa kasi kama Dumila ambao una wakazi zaidi ya 47,000;

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kwenda kupima, kupanga na kumilikisha maeneo hayo?

(b) Je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kuungana nasi baada ya Bunge kuja Wilaya ya Kilosa, kwa maana ya Jimbo la Kilosa na Mikumi, kwa ajili ya kuangalia migogoro ya ardhi ambayo inapelekea migogoro ya wakulima na wafugaji?

Name

Jerry William Silaa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukonga

Answer

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, Serikali imeshaelekeza maeneo yote siyo tu yanayokua kimiji kupangwa na kupimwa ili kuyatengenezea matumizi bora ya ardhi. Niungane mkono na Mheshimiwa Mbunge kwamba mji mdogo alioutaja unapaswa kufanyiwa mipango ya matumizi bora ya ardhi. Nimuombe tushirikiane katika kuangalia kama halmashauri yake imetenga fedha na pale Wizarani kama tuna uwezo kupitia Mradi wa KKK tuweze kufanya jambo hilo kwa haraka.

Mheshimiwa Spika, swali la pili baada tu ya Bunge hili la mwezi Februari ninayo ziara ya Jimbo la Kilombero kwa Mheshimiwa Asenga, uko mgogoro kule wa Baba Askofu, nikifanya ziara hiyo namuomba Mheshimiwa Mbunge mara baada ya kikao hiki tukutane tupange ratiba; tutapita na Wilaya ya Kilosa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji.

Name

Maimuna Ahmad Pathan

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DENNIS L. LONDO K.n.y. MHE. PROF. PALAMAGAMBA J. A. M. KABUDI aliuliza: - Je, lini Serikali itaandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi wa Jimbo la Kilosa kutokana na uwepo wa migogoro ya muda mrefu ya Wakulima na Wafugaji?

Supplementary Question 2

MHE. MAIMUNA A. PATHAN: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Kuna mgogoro mkubwa sana kati ya wakulima na wafugaji Mkoa wa Lindi kwenye Wilaya ya Liwale, Kilwa, Nachingwea na Mchinga unaopelekea kuuana na mashamba ya watu kuliwa na mifugo.

Je, Serikali ina mpango gani kabambe kutokomeza suala hili ili wananchi waishi kwa amani?(Makofi)

Name

Jerry William Silaa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukonga

Answer

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kuna tatizo kubwa la migogoro baina ya wakulima na wafugaji na katika Wilaya alizozitaja Mheshimiwa Mbunge za Liwale na Nachingwea Mkoani Lindi tatizo hili ni kubwa. Vilevile, lilijitokeza kwenye ziara ya Mheshimiwa Rais kwenye Mikoa ya Mtwara na Lindi.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kujipanga kupitia Wizara husika kwa maana Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Mifugo, Wizara ya Kilimo na Wizara ya TAMISEMI na itakuja na mpango kabambe wa kuhakikisha kadhia hii inaisha na wakulima na wafugaji wanaendelea kufanya shughuli zao katika matumizi bora ya ardhi bila ya kuingiliwa na kuleta machafuko na kuvunja amani.

Name

Zuena Athumani Bushiri

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DENNIS L. LONDO K.n.y. MHE. PROF. PALAMAGAMBA J. A. M. KABUDI aliuliza: - Je, lini Serikali itaandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi wa Jimbo la Kilosa kutokana na uwepo wa migogoro ya muda mrefu ya Wakulima na Wafugaji?

Supplementary Question 3

MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na migogoro kati ya Kata ya Makanya Ruvu na Makanya Bangalala ya muda mrefu. Je Serikali ina mpango gani wa kumaliza migogoro hii ya ardhi? Ahsante.
SPIKA: Hizo kata ziko wapi Mheshimiwa?

MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Same, Jimbo la Same Magharibi.

Name

Jerry William Silaa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukonga

Answer

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli wiki iliyopita nilipita Bangalala na Makanya na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Mheshimiwa David Mathayo. Tayari nimeunda timu ndogo itakwenda Bangalala na Makanya tarehe 07 ya mwezi huu na baada ya kuniletea taarifa nitafika tena kwenda kutoa majibu ya mgogoro huu ambao umekuwa ukiwasumbua wananchi kwenye mipaka yao.

Name

Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Primary Question

MHE. DENNIS L. LONDO K.n.y. MHE. PROF. PALAMAGAMBA J. A. M. KABUDI aliuliza: - Je, lini Serikali itaandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi wa Jimbo la Kilosa kutokana na uwepo wa migogoro ya muda mrefu ya Wakulima na Wafugaji?

Supplementary Question 4

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Katika eneo la Himo, maeneo yale ya Lokolova na mjini ilipokuwa estate ya sisal kuna mgogoro mikubwa na ambayo pia inazuia maendeleo ya pale. Je, Waziri atakubali kuenda na mimi Jimboni baada ya Mkutano huu ili aweze kutatua migogoro hii?(Makofi)

Name

Jerry William Silaa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukonga

Answer

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli mgogoro wa Lokolova pale Himo kwenye Jimbo la Mheshimiwa Dkt. Kimei ni mgogoro mkubwa baina ya Chama cha Ushirika na wakazi ambao wanadai kuwa ni wakazi wa asili wa eneo hilo. Mgogoro huu tayari taarifa yake imeshaandaliwa na tumeshakubaliana na Waziri wa Kilimo mara baada ya Bunge hili tutakwenda kwa pamoja kumaliza mgogoro huu uishe kabisa na usiendelee tena ili wananchi waweze kuendelea na shughuli zao za kiuchumi na kijamii.(Makofi)