Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Abeid Ighondo Ramadhani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Kaskazini

Primary Question

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mariam Kisangi, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais, wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwamba maeneo yote ambayo kuna miradi ya makampuni sheria ifuatwe ili waweze kupata ile huduma ya jamii kwa maana CSR. Kwa hiyo, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba sheria zipo kanuni zipo. Tutahakikisha kwamba Halmashauri ya Ilala pia inapata haki yake kutokana na ujenzi wa bomba hili la gesi, ahsante.

Supplementary Question 1

MHE. ABEID R. IGHONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi niulize maswali mawili madogo ya nyongeza. Kwanza, ninashukuru kwa maelezo mazuri ya Serikali ingawa hayajajibu swali langu la msingi kwamba ni lini maeneo haya ya utawala yatagawanywa?

Mheshimiwa Naibu Spika, tayari vikao vya wilaya kwa maana ya DCC pamoja na RCC vimeshakaa na kuleta mapendekezo Serikali. Kwa hiyo, nilitegemea nipate majibu sahihi hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa imebainika kwamba kuna gharama kubwa sana zinatumika katika kuendesha shughuli za Serikali kwenye kusimamia miradi, lakini kutokana na ukubwa wa maeneo haya Serikali ina mpango gani? Haioni haja ya kuongeza fedha kwa ajili ya usimamizi wa miradi kwenye maeneo yetu haya ikiwemo vyombo vya usafiri?(Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Abeid Ramadhani Ighondo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, sote Waheshimiwa Wabunge, ni mashuhuda kwamba Serikali hii ya Awamu ya Sita imefanya kazi kubwa sana ya kujenga miundombinu ya majengo ya utawala kwa maana ya Ofisi za Halmashauri, Ofisi za Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya, Vijiji na Kata, kazi hiyo bado inaendelea haijakamilika. Ndio maana Serikali imeweka kipaombele kwanza kukamilisha majengo ambayo tayari yanajengwa ili yatoe huduma vizuri. Baadaye tutakwenda kuanzisha maeneo mengine ya utawala ili tuhakikishe kwamba maeneo yaliyoanzishwa yanatoa huduma ipasavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tunafahamu uhitaji na ukubwa wa kijiografia ya maeneo haya. Mara Serikali itakapoanza kutoa kipaumbele katika kuanzisha maeneo mapya ya utawala tutawapa kipaumbele Halmashauri hii ya Singida.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, kuhusiana na ukubwa wa maeneo na kuongeza gharama ya usimamizi wa miradi ni kweli. Ndio maana Serikali inaendelea kupeleka vifaa vya usimamizi yakiwemo magari, pikipiki na kadhalika. Ninamhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kupitia mapato ya ndani tutaweka kipaumbele kwenye yale maeneo ambayo yana maeneo makubwa zaidi ya kijiografia na Serikali kuu tutaendelea kufanya hivyo, ahsante sana.

Name

Gibson Blasius Meiseyeki

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mariam Kisangi, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais, wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwamba maeneo yote ambayo kuna miradi ya makampuni sheria ifuatwe ili waweze kupata ile huduma ya jamii kwa maana CSR. Kwa hiyo, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba sheria zipo kanuni zipo. Tutahakikisha kwamba Halmashauri ya Ilala pia inapata haki yake kutokana na ujenzi wa bomba hili la gesi, ahsante.

Supplementary Question 2

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru, pamoja na mpango mzuri wa wa Serikali, kuna maeneo yanahitaji uangalizi wa haraka na muhimu sana kwa sababu athari zinazopatikana kutokana na jiografia kiutawala zinakuwa ni kubwa sana. Eneo kama la Gana Kitongoji kimoja kina watu zaidi ya 6,000 na kina visiwa zaidi ya vitano. Ni kwa nini Serikali isiangalie kwa umuhimu mkubwa kufanya mgawanyo wa maeneo haya sehemu Gana kwenye Kata ya Ilangala ili kuweza kurahisisha mazingira ya kiutawala kwenye maeneo haya? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. (Makofi)

Name

Gibson Blasius Meiseyeki

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Arumeru-Magharibi

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mkundi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba eneo la Gana, Ukerewe ni eneo ambalo lina visiwa vingi. Kwa hiyo, lina eneo kubwa la kijiografia na ni ngumu kuli-manage kiutawala Serikali inatambua hilo. Yote ni ya kwetu kukamilisha miundombinu katika maeneo ya utawala yaliyopo ni muhimu lakini pia, kuanzisha maeneo mapya ya utawala ni muhimu. Kwa hiyo, lazima tuweke kipaumbele ndio maana tumeanza na kipaumbele cha kukamilisha maeneo ya utawala yaliyopo na baadaye tutakwenda kwenye maeneo mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninamhakikishia Mheshimiwa Mkundi, kwamba tunafahamu hilo na Serikali italipa kipaumbele pale wakati utakapofika, ahsante.