Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Esther Lukago Midimu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga uzio katika Hospitali ya Mkoa wa Simiyu?
Supplementary Question 1
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri namshukuru sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha za ujenzi wa jengo la mama na mtoto tena ghorofa zuri na la kisasa. Mheshimiwa Rais, ahsante sana na Mwenyezi Mungu akubariki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niulize maswali yangu mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa vile Serikali imetenga bilioni mbili, napenda kujua ni lini fedha hizo zitaenda ili ujenzi uweze kuanza mara moja?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu ina upungufu wa watumishi, watumishi waliopo ni asilimia 40 upungufu ni asilimia 60. Ni lini Serikali itapeleka watumishi wa kutosha hasa madaktari bingwa wa ugonjwa wa moyo, magonjwa ya wanawake na magonjwa ya watoto? (Makofi)
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo anafuatilia hospitali yake lakini kwa uelewa wake kwamba kazi kubwa imeshafanyika kwenye Mkoa wa Simiyu kwenye eneo la hospitali yao ya mkoa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza ni lini fedha zitapelekwa. Mpaka sasa katika hospitali za mikoa ambazo ziko kwenye bajeti zimeshapelekewa hospitali nane. Nakuomba tuje tukae hapo tupige simu ili tupate tarehe ya uhakika lakini hakika fedha zinaenda kwa mwaka huu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ni kuhusu watumishi, moja Madaktari Bingwa, hilo halina mjadala, pia tutakaa kwa pamoja kwa sababu Waziri wa Afya ameshaelekeza ifanyike tathmini ya kujua Madaktari Bingwa waliopo nchi nzima na kuona ni wapi wako wengi nani wapi hawahitajiki halafu waweze kupelekwa maeneo mengine wakati tunangojea kupata kibali cha kuajiri wapya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia umezungumzia upungufu wa watumishi, ni kweli maeneo mengi kuna upungufu wa watumishi lakini niendelee kuwaambia Wabunge, wakati mwingine unaweza ukadhani kuna upungufu wa watumishi, lakini kuna maeneo mengi hasa kwenye hospitali zetu mpya ukienda unaweza kukuta hospitali ina watumishi 50 au 70 halafu wanakwambia kuna upungufu kwa kuangalia idadi ilivyopangwa kwenye utaratibu wa utumishi. Lakini ukiwauliza unakuta hospitali hiyo kwa siku wanaonekana wagonjwa 20 wakati kuna huo watumishi 70, maana yake upungufu unakuwa unasemwa kutokana na document za kiutumishi lakini sio halisi kwa maana ya mzigo ulioko kwenye eneo hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge wote tushirikiane kujua hilo, wakati mwingine katika hizi Hospitali zetu kubwa tukienda tuwaulize je, kwa siku mnawaona wagonjwa wangapi na nyie mko wa ngapi? Kwa namna hiyo tutajua jinsi ya kutumia resources vizuri.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved