Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Toufiq Salim Turky
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpendae
Primary Question
MHE. TOUFIQ SALIM TURKY aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga majengo ya viwanda kuwapangishia wawekezaji wazawa ili kuongeza idadi kwani gharama za kuanzisha kiwanda ziko juu?
Supplementary Question 1
MHE. TOUFIQ SALIM TURKY: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali na naomba kuuliza swali la nyongeza, tukijua kuwa malighafi nyingi ndani ya nchi yetu inatoka katika vijiji. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhamasisha sekta binafsi waweze kuwekeza hizo industrial pack ili wananchi waweze kunufaika katika Taifa lao hususani kwenye vijiji? Ahsante. (Makofi)
Name
Prof. Kitila Alexander Mkumbo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ubungo
Answer
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Kituo cha Uwekezaji pamoja na Mamlaka ya EPZA, tumeendelea kuhamasisha wawekezaji kupitia njia za makongamano na forum mbalimbali. Hivi ninavyozungumza wiki iliyopita tu, tulikuwa na wawekezaji wa ndani 200 na wawekezaji kutoka China 100, walikutana pamoja na kuweka mikakati ya kuweza kushirikiana kwenye kuwekeza katika haya makongamano makubwa. Kwa hivyo, niwakaribishe hata Waheshimiwa Wabunge akiwemo Mheshimiwa Toufiq ambaye ni mfanyabiashara muhimu kabisa katika nchi yetu, aweze kuwekeza katika maeneo hayo. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved