Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Bahati Keneth Ndingo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Mbarali
Primary Question
MHE. BAHATI K. NDINGO aliuliza:- Je, lini Serikali itawalipa mafao wastaafu wa Shamba la Kapunga Wilayani Mbarali lililokuwa linamilikiwa na NAFCO?
Supplementary Question 1
MHE. BAHATI K. NDINGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na naomba kuuliza swali moja tu la nyongeza; tathmini tayari ilishafanyika Mheshimiwa Naibu Waziri na mpaka barua Wizara ya Fedha ilienda na wazee hawa wapo 65, na wanachokidai Serikalini ni shilingi milioni 261. Naomba commitment ya Serikali juu ya hili kwa sababu ni suala la muda mrefu. (Makofi)
Name
Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Iramba Magharibi
Answer
WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mbunge makini kabisa wa Mbarali kwa jinsi anavyofuatilia masuala ya wananchi wake na kwa kweli hawakukosea kumchagua.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tumepokea mahitaji haya yanayohusu wazee wetu wa Mbarali sambamba na baadhi ya maeneo mengine kama Mbunge alivyohitaji commitment nimuombe tu aridhie nimelichukua tukio hapa hapa Bungeni nitampa status ikiwezekana tukiweza kulikamilisha kabla hajarudi, akirudi awape taarifa tu.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved