Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Noah Lemburis Saputi Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Magharibi
Primary Question
MHE. EMMANUEL L. SHANGAI aliuliza: - Je, lini Serikali itatenga fedha za kutosha kwa ajili ya kumalizia Mradi wa Maji wa Mageri utakaohudumia vijiji nane Wilayani Ngorongoro?
Supplementary Question 1
MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Katika Jimbo la Arumeru Magharibi, baadhi ya miradi mingi ya maji imesimama kwa Wakandarasi kukosa malipo; je, Serikali ina mkakati gani wa kupeleka fedha kwa ajili ya miradi ya maji ikiwemo Mradi wa Olmulo katika Kata ya Oljoro?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Lemburis, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, malipo kwa Wakandarasi, tayari tumeanza kuwaondoa Wakandarasi kwenye foleni ya malipo mara baada ya kupatiwa fedha za Desemba na Januari. Kwa hiyo, hata kwa mradi huu kwenye Jimbo lake naye, Mkandarasi huyu atalipwa ili aweze kuendelea na kazi ili amalize kazi hii kwa wakati, wananchi wapate maji safi na salama.
Name
Agnes Elias Hokororo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. EMMANUEL L. SHANGAI aliuliza: - Je, lini Serikali itatenga fedha za kutosha kwa ajili ya kumalizia Mradi wa Maji wa Mageri utakaohudumia vijiji nane Wilayani Ngorongoro?
Supplementary Question 2
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni lini Serikali itachimba visima kwenye maeneo ambayo hakuna vyanzo vya maji katika Mkoa wa Mtwara?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Agnes Hokororo, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Agnes Hokororo, ameshafuatilia mara nyingi na kuelezea namna wanawake wa Mkoa wa Mtwara, baadhi ya maeneo wanavyopata shida, lakini tumeshaanza kuchimba visima. Maeneo mengine ambayo bado yana uhitaji wa kuchimbiwa visima yapo kwenye mkakati. Nimwambie Mheshimiwa Hokororo, tutakutana na kuona kwamba tunapanga ratiba nzuri ya kuweza kufika maeneo haya. (Makofi)
Name
Yahya Ally Mhata
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyumbu
Primary Question
MHE. EMMANUEL L. SHANGAI aliuliza: - Je, lini Serikali itatenga fedha za kutosha kwa ajili ya kumalizia Mradi wa Maji wa Mageri utakaohudumia vijiji nane Wilayani Ngorongoro?
Supplementary Question 3
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Naibu Spika, jina langu ni Yahya Mhata, Mbunge wa Nanyumbu.
Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya yetu ya Nanyumbu tuliingia Mkataba na Mkandarasi kwa ajili ya usambazaji wa maji kutoka Bwawa la Maratane katika vijiji vinne. Sasa hivi ni mwaka mmoja Mkandarasi hayupo site na hajaanza kazi, nini kauli ya Serikali? (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Yahya, Mbunge wa Nanyumbu, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, hili suala naomba niwe nimelipokea na nitalifuatilia Mheshimiwa Mbunge, kuhakikisha hii kazi inakamilika.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved