Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Robert Chacha Maboto
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda Mjini
Primary Question
MHE. ROBERT C. MABOTO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kumaliza changamoto ya uvuvi haramu katika Ziwa Victoria?
Supplementary Question 1
MHE. ROBERT C. MABOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwanza nampongeza Mheshimiwa Rais, kwa kazi kubwa ambayo ameendelea kuifanya kwenye sekta ya uvuvi. Hata hivyo nina swali moja la nyongeza. Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wananchi wa Kata yangu ya Nyatwali na Bunda kwenye suala la ufugaji wa samaki wa vizimba? Ahsante. (Makofi)
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema kwamba Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, tayari imesharuhusu waombaji waendelee kuomba vizimba na hata maboti. Kwa hiyo, kwa kesi ya Mheshimiwa Maboto, nimshauri awahamasishe Wavuvi wake waonane na Maafisa Uvuvi, wawasaidie kuandika maandiko mazuri yatakayowasaidia kupata mikopo hiyo ili waweze kupata hizo nyenzo za uvuvi.
Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba Mheshimiwa Maboto, baada ya Bunge hili tuonane nimwelekeze, nimpe mawasiliano ya wanaohusika na habari hii ili waweze kumsaidia kuandika maandiko mazuri yatakayomsaidia kupata mkopo.
Name
Francis Kumba Ndulane
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kaskazini
Primary Question
MHE. ROBERT C. MABOTO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kumaliza changamoto ya uvuvi haramu katika Ziwa Victoria?
Supplementary Question 2
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ina mkakati gani wa kudhibiti uvuvi haramu katika Wilaya ya Kilwa?
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema katika jibu la msingi kwamba Serikali inakusudia kuanzisha chombo maalum kitakachosimamia, kwa sababu habari hii ya uvuvi haramu imekuwa ni suala mtambuka, kila maeneo, kila sehemu uvuvi haramu umetamalaki, sasa Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, tumekuja na mkakati maalum wa kuanzisha chombo maalum kitakachosimamia wavuvi na shughuli zote za uvuvi ikiwa ni pamoja na uvuvi haramu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kwenye eneo la Wilaya hiyo, Serikali itakapoanzisha chombo hiki kitakuwa na mamlaka ya kusimamia maeneo yote nchi nzima yanayohusiana na masuala ya uvuvi, ahsante.
Name
Jafari Chege Wambura
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Rorya
Primary Question
MHE. ROBERT C. MABOTO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kumaliza changamoto ya uvuvi haramu katika Ziwa Victoria?
Supplementary Question 3
MHE. JAFARI W. CHEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa kwangu Wilaya ya Rorya tayari zaidi ya vikundi nane vimeshaandika andiko kwa ajili ya kupewa vizimba na boti; je, ni lini vikundi hivi vitapatiwa mahitaji haya?
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama vikundi hivyo tayari vimeshaomba na tayari vimeshafanyiwa assessment, awamu ya kwanza alifanya Mheshimiwa Rais hivi majuzi, awamu ya pili tunaenda. Kama tayari wameshakidhi vigezo watapatiwa vizimba hivyo.
Name
Salma Rashid Kikwete
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Mchinga
Primary Question
MHE. ROBERT C. MABOTO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kumaliza changamoto ya uvuvi haramu katika Ziwa Victoria?
Supplementary Question 4
MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kama ambavyo amezungumza Naibu Waziri kuhusiana na suala la kuomba vizimba na maboti, sisi kama Jimbo la Mchinga, tumeshaomba vizimba na tumeshaomba maboti; je, Serikali inatuambiaje juu ya jambo hili? (Makofi)
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa maeneo ambayo tayari wavuvi wameshaomba vizimba, sasa tunakwenda kwenye mgao wa awamu ya pili ambao hivi karibuni tutaanza mgao huo. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kama vikundi vyake tayari vimekidhi vigezo na masharti yaliyowekwa na Benki yetu ya Kilimo, tutaenda kuwapatia vizimba hivyo.
Name
Furaha Ntengo Matondo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ROBERT C. MABOTO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kumaliza changamoto ya uvuvi haramu katika Ziwa Victoria?
Supplementary Question 5
MHE. FURAHA N. MATONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. Je, ni lini Serikali itatoa mafunzo kwa vikundi vya BMU (Beach Management Unit) kwa ajili ya kuwa na nguvu ya kuzuia uvuvi haramu?
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, tayari Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeshaanza kutoa mafunzo kwenye vikundi vya BMU. Kama Mheshimiwa Mbunge ana kikundi ambacho pengine kinahitaji mafunzo hayo, tuko tayari kwenda kumfundisha, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved