Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Rashid Abdallah Shangazi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mlalo
Primary Question
MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. ELIBARIKI I. KINGU aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Mahaya – Singida?
Supplementary Question 1
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Kama nilivyosema, shule hii inaitwa Mayaha, naomba hiyo isahihishwe lakini nina swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Halmashauri ya Lushoto ziko shule kongwe ambazo zimejengwa tangu miaka ya 1950. Shule hizo ni Mbaramo, Fufui, Lwandai, Lunguza na Tema.
Je, Serikali ina mpango gani mahususi shule hizi ambazo si za zamani tu pia ni kongwe na nyingi zimejengwa kwa miti ziweze kufanyiwa ukarabati?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, jambo la kwanza tumepokea hayo marekebisho na kama yalivyoingia katika Hansard ndivyo ambavyo fedha zitakwenda katika maeneo hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili katika shule ambazo Mheshimiwa Mbunge amezitaja za Mbaramo, Fufui, Nyasa, Lwandai, Lunguza na Tema ambazo zimejengwa karibu miaka ya 60 na zinahitaji marekebisho makubwa; kikubwa ambacho Mheshimiwa Mbunge atambue kwamba, Serikali sasa hivi inaendelea na Mradi wake wa BOOST ambao umekusudia kukarabati shule kongwe nchini ikiwemo hizi ambazo amezitaja. Kwa hiyo kila mwaka Serikali itaendelea kuziweka katika bajeti ili kuzirekebisha. Kwa hiyo Mheshimiwa Mbunge wathibitishie tu wananchi wako kwamba Serikali ipo kazini na itazifanyia kazi.
Name
Cosato David Chumi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafinga Mjini
Primary Question
MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. ELIBARIKI I. KINGU aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Mahaya – Singida?
Supplementary Question 2
MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi, pamoja na jitihada nyingi ambazo Serikali inafanya kujenga madarasa na shule mpya, kwa mfano Mafinga tumejengewa shule mpya kabisa pale Mwongozo.
Je, Serikali iko tayari kama ilivyofanya katika program ya shule kongwe za Serikali kuja na mpango maalum kwa kufanya ukarabati mkubwa katika shule kongwe za msingi, kama Shule ya Msingi Mafinga, Mkombwe, Wambi nakadhalika?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, Serikali ina mpango huo kuhakikisha kwamba inakarabati shule zote kongwe za msingi ikiwemo Shule ya Mafinga na Mkombwe ambayo ameitaja Mheshimiwa Mbunge, kwa hiyo hilo lipo katika mipango ya Serikali.
Name
Grace Victor Tendega
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. ELIBARIKI I. KINGU aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Mahaya – Singida?
Supplementary Question 3
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Shule ya Msingi Kimala na Shule ya Msingi Nyawegete ambazo zipo katika Jimbo la Kilolo ni shule ambazo zimechoka mno zinahitaji ukarabati mkubwa sana.
Je, Serikali ina mpango upi wa kujenga upya madarasa katika shule hizo?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango wa Serikali ni kuhakikisha shule zote kongwe nchini zinafanyiwa ukarabati, ikiwemo Shule ya Kimala na Nyawegete ambayo Mheshimiwa Mbunge ameielezea hapa ahsante.
Name
Joseph Michael Mkundi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ukerewe
Primary Question
MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. ELIBARIKI I. KINGU aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Mahaya – Singida?
Supplementary Question 4
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Kwa kuwa Shule ya Msingi Gana iliyoko kwenye Kisiwa cha Gana Jimboni Ukerewe ina upungufu mkubwa sana wa miundombinu. Ni kwa nini Serikali isione umuhimu wa kulifanya eneo hili kama eneo maalum ikatenga pesa kwa ajili ya kufanya ukarabati mkubwa? Nashukuru.
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, maeneo yote ambayo yana mahitaji makubwa ikiwemo katika Jimbo la Ukerewe katika Shule ya Msingi Gana Serikali imeendelea kuiweka katika kipaumbele kupitia halmashauri vilevile kupitia fedha kutoka Serikali Kuu, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved