Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Edward Olelekaita Kisau
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kiteto
Primary Question
MHE. EDWARD O. KISAU K.n.y. MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Skimu za Umwagiliaji katika Tarafa za King’ori na Mbuguni pamoja na eneo la Kusini mwa Tarafa ya Poli – Arumeru Mashariki?
Supplementary Question 1
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Nina maswali mawili ya nyongeza. Ni lini utakuwa tayari kutembelea Jimbo la Arumeru Mashariki kukagua skimu za umwagiliaji alizotaja Mheshimiwa Mbunge hapa?
Swali la pili, katika mwaka wa fedha uliopita Wizara ya Kilimo, Mradi wa Umwagiliaji wa Ngipa, Engusero-Kiteto ulipitishwa, ni lini sasa mtaanza kujenga?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, niko tayari kutembelea hizo skimu, katika moja ya weekend tuombe ruhusa tu kwa Mheshimiwa Spika kama nilivyoahidi kwa Mheshimiwa Abubakari Asenga, tukafanye kazi. Nguvu tunayo na uwezo wa kufanya hiyo kazi tunao, Mheshimiwa Dkt. Samia ametuamini.
Mheshimiwa Spika, kuhusu Skimu ya Ngipa ambayo ilikuwepo katika mwaka wa fedha uliopita, nina uhakika Tume ya Taifa ya Umwagiliaji iko katika hatua za mwisho za kumpata mkandarasi ili iweze kufanyiwa kazi, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved