Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Zuberi Mohamedi Kuchauka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Liwale
Primary Question
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza: - Je, Serikali ipo tayari kuleta wataalamu Liwale kufanya utafiti kujua chanzo cha ugonjwa wa majani ya mikorosho kunyauka? (Makofi)
Supplementary Question 1
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna aina nyingi sana ya viuatilifu madukani ukiacha vile viuatilifu ambavyo vinatolewa ruzuku na Serikali, lakini kwenye aduka kuna viuatilifu vingi sana ambavyo zinachanganya wakulima na kupunguza uzalishaji wa mazao haya ya korosho. Je, Serikali ina mkakati gani wa kufuatilia kuhakikisha viuatilifu vinavyopatikana kwenye maduka hayo vyote vina ubora unaofanana? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, wapo wasafirishaji waliosafirisha pembejeo zile za ruzuku kutoka kwenye Vyama vyetu Vikuu kwenda kwenye Vyama vya Msingi. Leo ni mwaka mzima sasa hivi hawajalipwa na tayari benki wameanza kuwafilisi. Nini kauli ya Serikali kuwasaidia wasafirishaji wale ili kuwapatia fedha zao wakalipa kwenye madeni Serikalini na benki? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, jambo la kwanza, nampongeza vilevile Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia mambo makubwa ya msingi katika sekta ya kilimo. Nimwondoe shaka tu kwamba, tunatambuka kwamba kuna viuatilifu vingi katika maduka, lakini viuatilifu karibu vyote kabla havijaingia katika maduka tuna mamlaka zetu nchini ikiwemo TPHPA pamoja na TBS ambazo zimekuwa zikithibitisha ubora wake na kila wakati tumekuwa tukifanya control kwa kupitia na kukagua. Kwa hiyo, tutaendelea kulifuatilia hili ili kuhakikisha kwamba vigezo vyote na masharti yanazingatiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu wasafirishaji hususani wa zao la korosho, ninaiagiza Bodi ya Korosho kuhakikisha kwamba kabla hatujafunga mwisho wa mwaka huu wa fedha wawe wamewalipa wasafirishaji hawa kwa ajili ya kuondokana na madeni ambayo wamekuwa nayo katika benki, ahsante. (Makofi)
Name
Fatma Hassan Toufiq
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza: - Je, Serikali ipo tayari kuleta wataalamu Liwale kufanya utafiti kujua chanzo cha ugonjwa wa majani ya mikorosho kunyauka? (Makofi)
Supplementary Question 2
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo lililopo Jimboni Liwale linafanana na tatizo lililopo katika baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Dodoma, mimea ya mahindi ilikauka katika msimu huu. Nini kauli ya Serikali kutokana na kadhia hii? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwamba changamoto yoyote inapotokea sisi Wizara ya Kilimo kupitia mamlaka yetu ya utafiti TARI huwa tunaiagiza kwenye eneo husika na kufanya tafiti ili kugundua ukubwa wa tatizo ama tatizo limetokana na nini na kilichotokea Dodoma, tulishaiagiza TARI na inaendelea na utafiti, wakishamaliza tutaleta matokeo na tutamjulisha Mheshimiwa Mbunge, ahsante.
Name
Tunza Issa Malapo
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza: - Je, Serikali ipo tayari kuleta wataalamu Liwale kufanya utafiti kujua chanzo cha ugonjwa wa majani ya mikorosho kunyauka? (Makofi)
Supplementary Question 3
MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, mikorosho imekuwa ikikumbwa na magonjwa mengi na inaonekana kama yameshindwa kutibika; je, Serikali sasa iko tayari kushirikiana na watafiti ikiwezekana hata wa kutoka nje ya nchi ili kutatua changamoto hiyo ya magonjwa na kuongeza tija kwa wakulima ambao wamekuwa wakilima lakini wanapata tija ndogo? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwamba Serikali tuko tayari kushirikiana na mdau yeyote kuja kufanya tafiti hapa nchini awe anatoka nje ya nchi au taasisi yoyote ndani ya nchi tuko tayari kufanya nao lakini kwa kuzingatia masharti na sheria za nchi yetu, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved