Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Conchesta Leonce Rwamlaza

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza mgogoro wa ardhi wa Rwanyabara baina ya mwekezaji na wananchi wa Kijiji cha Bushasha Bukoba Vijijini?

Supplementary Question 1

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro huu ni wa muda mrefu na Serikali ya Mkoa na Wilaya ina taarifa ya mgogoro huu na walishindwa kuukamilisha mpaka wakafika hatua hii. Mimi nasema kwamba kwa hatua ambayo Serikali inapanga kwamba sasa wamalize huu mgogoro ambao ni wa kijamii, mtu hawezi akawa na eka 240 akidai ni chifu na huku wanakijiji wanadai ni mali ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naitaka sasa Wizara yenyewe kwa sababu mmekuwa mnaonesha kumaliza migogoro hii, sasa mwende ninyi wenyewe mkasaidie hawa watu wa Mkoa na Wilaya ambao walishindwa kwa muda mrefu. Mwende mkahakikishe mnamaliza mgogoro huu ili mwekezaji apate eneo lake na wanakijiji wapate eneo lao waweze kukaa kwa amani, ahsante.

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ushauri uliotolewa na Mheshimiwa Mbunge tunauchukua na tunakwenda kuufanyia kazi. Nimwahidi tu Mheshimiwa Mbunge tutakwenda huko kwenye eneo la tukio ili tuone kwa kushirikiana na Mkoa tunamalizaje jambo hilo.