Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Tamima Haji Abass

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TAMIMA HAJI ABASS aliuliza:- Je, lini Serikali itatunga sheria mahsusi kwa makosa ya ukatili wa kijinsia?

Supplementary Question 1

MHE. TAMIMA HAJI ABASS: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwa majibu hayo, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, ni kigezo gani cha kubainisha haja ya kuwa na sheria mahususi ya makosa ya ukatili wa kijinsia? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia vinazidi kushamiri nchini na sheria zipo, je, Serikali inatumbia nini kuhusiana na hali hiyo? Ahsante. (Makofi)

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu vigezo gani vinafaa ili iweze kuandikwa sheria moja, nimejibu katika swali la msingi kwamba ni tathmini ya uzito au ukengeufu unaosababisha na mtawanyiko wa sheria hizi hususani zikishafanyika na Tume ya Marekebisho ya Sheria then Serikali inashauriwa ipasavyo. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge utupe nafasi kama Serikali kupitia Tume yetu ya Kurekebisha Sheria ambayo inahusisha wadau mbalimbali wakiwemo Wabunge tutapata msimamo wa pamoja wa namna ya kuliendea jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kuendelea kushamiri kwa matendo ya ukatili wa kijinsia, nichukue nafasi hii kuiasa jamii kwa ujumla wake kuzingatia maadili ya jamii, kwa sababu karibu Tanzania ambayo ina mila, desturi, dini mbalimbali hakuna hata moja inayoruhusu mambo haya kufanyika, lakini maadamu yanafanyika kwenye jamii zetu, niiase pale inapotokea wahusika watoe taarifa kwenye vyombo vyetu vya usimamizi wa sheria ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwafikisha wahalifu hao kwenye mahakama zetu, nashukuru.

Name

Francis Kumba Ndulane

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. TAMIMA HAJI ABASS aliuliza:- Je, lini Serikali itatunga sheria mahsusi kwa makosa ya ukatili wa kijinsia?

Supplementary Question 2

MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, je, ni lini Serikali itakarabati Mahakama za Mwanzo katika Tarafa ya Kipatimu, Miteja na Njinjo? (Makofi)

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nilijibu wakati nitakapo jibu swali la ujenzi wa Mahakama ambalo litafuta muda mfupi ujao.

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la Mheshimiwa Ndulane aliyeuliza umuhimu wa karabati, kwa maana ya kukarabati Mahakama zilizochakaa, tunalichukua hili na hivi sasa Mahakama ipo kwenye mkakati wa awamu ya pili ya ujenzi na ukarabati wa mahakama zote kongwe na pale ambapo bajeti itakavyoruhusu, kwa kweli nia ya Mahakama ni kukarabati mahakama zote ili zifikie kiwango cha kutoa haki kwa wananchi kwa mazingira ambayo niwezeshi yanaweza kutumia ICT na vitu kama hivyo.

Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge tuwe na matumaini, fedha zikipatikana Mahakama zetu zote zitakarabatiwa, ahsante sana. (Makofi)

Name

Mwantum Dau Haji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TAMIMA HAJI ABASS aliuliza:- Je, lini Serikali itatunga sheria mahsusi kwa makosa ya ukatili wa kijinsia?

Supplementary Question 3

MHE. MWANTUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona, Serikali itunge sheria haraka ili wabakaji waache ukatili huu.

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeeleza katika jibu la msingi kwamba zipo sheria maeneo mbalimbali ambazo yoyote kati ya sheria hizo inaweza ikatumika kuwadhibiti watu wanaofanya matendo ya ukatili wa kijinsia. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nimshauri tu ikiwa mambo yamefanyika kwenye masuala ya mitandao tutatumia Sheria ya Mitandao, ikiwa amefanyiwa mtoto ipo Sheria ya Mtoto na masuala mengine, ninashukuru.