Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Francis Kumba Ndulane
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kaskazini
Primary Question
MHE. FRANCIS K. NDULANE K.n.y. MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza:- Je, upi mpango wa Serikali wa kuipatia gari la Zimamoto Wilaya ya Liwale ili kukabiliana na majanga ya moto?
Supplementary Question 1
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Mwenyekiti, jeshi hili la Zimamoto ni la muhimu sana na limekuwa likifanya kazi kubwa sana, hasa kwenye Mkoa wetu wa Lindi, ikiwemo kudhibiti na kupambana na mafuriko yanayoendelea katika Mkoa wa Lindi. Hata hivyo, jeshi hili hawana Ofisi nzuri za kufanyia kazi.
MWENYEKITI: Swali la nyongeza Mheshimiwa Francis.
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali ina mkakati gani wa kukarabati Ofisi za Zimamoto zilizopo katika Wilaya za Mkoa wa Lindi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, watumishi wa Ofisi za Zimamoto wamekuwa hawana nyumba za kuishi. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwajengea nyumba za kuishi katika Mkoa wa Lindi?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Francis Ndulane kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza linalohusiana na ukarabati wa ofisi, kadiri Serikali itakavyopata fedha itatenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa Ofisi za Zimamoto na Uokoaji katika maeneo aliyotaja Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Liwale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu nyumba za makazi ya Askari, kama nilivyosema kwenye jibu la msingi, ni kwamba kadri Serikali itakavyopata fedha itatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari wetu wa zimamoto na askari wengine hapa nchini, ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved