Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mussa Ramadhani Sima
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Mjini
Primary Question
MHE. MUSSA R. SIMA K.n.y. MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itajenga ofisi za Mamlaka ya Mapato – TRA katika Wilaya ya Mkalama?
Supplementary Question 1
MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri, lakini nina swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa, ziko ofisi za muda zinatumiwa katika Wilaya ya Mkalama pale na maafisa wa TRA na wakimaliza kazi wanarudi kwenye Wilaya ya Iramba.
Je, wakati wanasubiri kujenga ofisi zao kamili, Serikali haioni haja sasa ya kuweka wafanyakazi wakawepo kwa muda wote hapo Wilaya ya Mkalama? (Makofi)
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mussa Sima. Kabla ya kujibu swali hilo naomba nimpongeze sana kwa juhudi zake katika kuwatetea wananchi wa jimbo lake. Serikali itaangalia uwezekano wa kuweka watumishi wa kudumu wakati wa kusubiria ujenzi huo wa ofisi katika eneo husika, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved