Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Priscus Jacob Tarimo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Mjini
Primary Question
MHE. PRISCUS J. TARIMO aliuliza:- Je, upi mpango wa kurejesha TFDA kwani imeacha masuala ya chakula na inakinzana na utaratibu wa usimamizi wa chakula na madawa duniani?
Supplementary Question 1
MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa kuwa, tayari imeshaonesha kwamba, TBS imeshindwa kushughulikia masuala ya chakula na kwa kuwa, Kamati mbalimbali za Bunge, Kamati ya Afya imetoa mapendekezo masuala haya ya chakula yapelekwe TMDA, lakini Kamati nyingine zimesema irejeshwe TFDA na kwa kuwa, practice duniani ni Food and Drugs Authority, ni kwa nini mchakato huo usifanyike kwa haraka zaidi? (Makofi)
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge wa Moshi kwa sababu, kwa muda mrefu huko nyuma, Moshi haikuwahi kupata Mbunge mzuri kama huyu anayejua Wanamoshi wanataka nini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa swali lake ambalo kimsingi ni swali moja la mwisho, ni kwamba, kwa sababu hili jambo limepitishwa na Bunge letu Tukufu na Bunge ni organ kubwa muhimu sana, tunaomba kwa sababu Serikali inaendelea na huo mchakato, tuendelee kufuata taratibu zote ambazo zilifuatwa huko nyuma, halafu hili jambo litakuja Bungeni kama maelekezo ya Kamati yalivyoelekeza kwa Serikalini kwanza kukubaliana na kuweka mambo sawa kabla ya kulileta Bungeni kabla halijaiva vizuri. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved