Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Marwa Ryoba Chacha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Serengeti

Primary Question

MHE. MARWA R. CHACHA aliuliza:- Wananchi wa Serengeti wamekuwa wakiathirika sana na wanyamapori hususan tembo ambao huharibu na kula mazao ya wananchi katika mashamba yao na kuikosesha Halmashauri mapato:- (a) Je, Serikali itarejesha chanzo cha mapato yaani bed fee na sehemu ya gate fee kwa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti? (b) Makampuni mengi ndani ya hifadhi yanagoma kulipa ushuru wa huduma (service levy) kwa Halmashauri. Je, Serikali inaisaidiaje Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kupata ushuru huu wa huduma?

Supplementary Question 1

MHE. MARWA R. CHACHA: Nina maswali mawili. Kwanza, naomba niwaambie tu kwamba Serengeti wanaishi binadamu, siyo wanyama peke yake.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukija Serengeti ni aibu sana, yaani utafikiri haipo Tanzania. Hatuna maji, hatuna lami, hatuna chochote, yaani faida tunayoipata sisi kuishi Serengeti National Park ni tembo kula mazao ya wananchi na kuua watu. Hiyo ndiyo faida tunayoipata.
Sasa mimi nimeuliza kwamba kwanini Wizara tusipate sehemu ya gate fee au bed fee? Hivyo vilikuwa ni vyanzo vya mapato vya Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti. Kwa sasa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti haina chanzo chochote. Ukija kwenye kwenye service levy, wamechukua vyote, hakuna kitu. Sasa sisi own source tunatoa wapi? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia kwenye maelezo ya Naibu Waziri, amesema kwamba wamewahi kuisaidia Wilaya, mimi nimekuwa Diwani tangu mwaka 2010 sijaona mradi wowote wa TANAPA.
MHE. MARWA R. CHACHA: Swali la kwanza, kwa kuwa ni majirani zetu, ninyi watu wa TANAPA naomba mtujengee game post kila kata katika kata kumi, ili kuzuia tembo, sisi tulime tu, hamna shida. Tunahitaji game post. Hata gari la kufukuzia tembo hatuna.
Swali la pili.

MHE. MARWA R. CHACHA: Swali la pili, kwa kuwa sasa makampuni haya yameenda Mahakamani kuishitaki Serikali, Mwanasheria wetu unasemaje kuhusu hili? Maana sasa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti hatuna own source? (Makofi)

Name

Prof. Jumanne Abdallah Maghembe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanga

Answer

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, kuacha siku nyingine, jana nilikaa na wananchi wa Serengeti katika ofisi yangu wakiandamana na Mheshimiwa Mbunge kuelezea tatizo la single entry katika Pori la Serengeti ili ifanyiwe marekebisho, wananchi wa Serengeti ambao wana WMA waweze kufaidika zaidi na pori la Serengeti.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimewasikiliza na tatizo lao tuko kwenye hatua ya kulitatua. Kwa hiyo, siyo kweli kwamba wananchi wa Serengeti hawafaidiki na kitu chochote.
Mheshimiwa Naibu Spika, vijiji vilivyo na hizi WMA ambavyo vinapakana na Serengeti vinapata shilingi milioni 300 kila mwezi kutokana na biashara ya WMA hizi. Kwa hiyo, siyo kweli kabisa kwamba hawafaidiki na kitu chochote.
Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, tuko tayari kuongeza ulinzi katika maeneo ya mipaka na katika mwaka huu unaokuja wa fedha tumepanga tujenge vibanda vitatu kwa ajili ya askari ili kuhakikisha kwamba tunasaidiana na Wilaya katika kuwalinda wananchi na hivi sasa tayari tuna magari ambayo yanazunguka kule kuhakikisha kwamba tunasaidia kupunguza hasara ambazo wananchi wanaweza kupata kutokana na wanyama waharibifu.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kushirikiana na Wilaya ili kuhakikisha kwamba tunapunguza madhara haya.

Name

Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Primary Question

MHE. MARWA R. CHACHA aliuliza:- Wananchi wa Serengeti wamekuwa wakiathirika sana na wanyamapori hususan tembo ambao huharibu na kula mazao ya wananchi katika mashamba yao na kuikosesha Halmashauri mapato:- (a) Je, Serikali itarejesha chanzo cha mapato yaani bed fee na sehemu ya gate fee kwa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti? (b) Makampuni mengi ndani ya hifadhi yanagoma kulipa ushuru wa huduma (service levy) kwa Halmashauri. Je, Serikali inaisaidiaje Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kupata ushuru huu wa huduma?

Supplementary Question 2

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kuniona.
Naomba kumwuliza Waziri, kwa kuwa mbuga ya Hifadhi ya Mkomazi iko katika Wilaya za Same, Mwanga na Lushoto na kwa kuwa lengo la hifadhi hizi ni kuongeza Pato la Taifa. Je, ni lini Serikali itajenga mlango wa kuingilia katika mbuga ya Hifadhi ya Mkomazi katika eneo la Kivingo, Kata ya Lumbuza ili na Wilaya ya Lushoto nayo iweze kuchochea Pato la Taifa? Ahsante.

Name

Prof. Jumanne Abdallah Maghembe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanga

Answer

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara yangu inafanya study hivi sasa ya kuangalia namna ya kuongeza milango ya kuingia katika Pori la Mkomazi na iko tayari kufungua mlango wa kuingia Mkomazi kutoka katika Jimbo la Mheshimiwa Mbunge.