Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Maryam Azan Mwinyi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Chake Chake
Primary Question
MHE. MARYAM AZAN MWINYI aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kusimamia uhifadhi wa misitu ikizingatiwa kwamba imeandaa na kuzindua biashara ya hewa ya ukaa?
Supplementary Question 1
MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa wananchi wengi hawana uelewa wa biashara ya kaboni, je, Serikali ina mkakati gani wa kuimarisha biashara hiyo ya kaboni Tanzania Bara na Zanzibar?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kumekuwa na kampeni endelevu ya upandaji miti nchini, je, kampeni hii inakidhi utunzaji wa mazingira? (Makofi)
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuhakikisha kwamba elimu hii inatolewa, Ofisi ya Makamu wa Rais imekuwa na jukumu la kusimamia jambo hili na kwa mahsusi kabisa Kituo cha Taifa cha Uratibu wa Usimamizi wa biashara hii inafanya kazi kubwa ya kuwaelimisha wananchi na kama mnavyofahamu tayari Serikali ilitunga kanuni za usimamizi na udhibiti wa biashara ya kaboni ya mwaka 2022. Niwaombe wadau wetu wapate fursa ya kutembelea kwenye kituo chetu cha Taifa cha Uratibu na Usimamizi ili kupata taarifa za msingi za jinsi ya kuweza kushiriki kwenye biashara hii.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved