Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ndaisaba George Ruhoro
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ngara
Primary Question
MHE. NDAISABA G. RUHORO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa vibali vya misimu katika Ofisi za Uhamiaji ngazi za wilaya?
Supplementary Question 1
MHE. NDAISABA G. RUHORO: Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wengi wa mipakani wakiwepo wananchi wa Wilaya ya Ngara wamekuwa wahanga wa maswahibu kadha wa kadha yanayowakuta kutokana na changamoto za kutofahamu sheria hii na taratibu hizi za vibali vya misimu.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni upi mkakati wa Serikali wa kupeleka elimu Ngara na maeneo mengine ya mipakani ili wananchi wajue taratibu za kupata vibali vya msimu kwa raia wa kigeni? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na mkakati wa elimu, kwanza, tunaandaa utaratibu wa Uongozi wa Jeshi la Uhamiaji Tanzania na Jeshi la Uhamiaji la nchi jirani kwa upande wa mpakani mwa Jimbo la Mheshimiwa Mbunge, nadhani itakuwa ni nchi ya Burundi. Tunaamini kabisa Serikali za nchi husika zina wajibu na umuhimu mkubwa sana wa kuelimisha wananchi wao kutambua juu ya taratibu za kuweza kupata vibali hivyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano miongoni mwa changamoto ambazo zinakabiliana na utoaji wa vibali hivi ni wananchi kukosa elimu juu ya umuhimu au haja ya kuwa na hati za kusafiria katika nchi zao. Kwa hiyo, wengi walikuwa wakija wanakuwa hawana hati za kusafiria na hivyo kuleta usumbufu usiyokuwa wa lazima.
Kwa hiyo, jitihada hizo na mkakati huo umeshaandaliwa kati ya chombo cha uhamiaji cha nchi yetu na vyombo vya nchi jirani ili watusaidie kutoa elimu katika nchi yao, wakati Jeshi la Uhamiaji na Serikali kwa ujumla ikiendelea na jitihada zake za kutoka elimu kwa wananchi wa nchi yetu hasa wanaoishi katika maeneo ya mpakani.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved