Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Neema Kichiki Lugangira
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NEEMA K. LUGANGIRA aliuliza: - Je, lini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi zitakuwa tayari baada ya makosa ya ukatili wa kijinsia kuongezwa kwenye Sheria za Uchaguzi?
Supplementary Question 1
MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa maelezo mazuri ya Serikali na natambua kwamba Kanuni za Maadili ya Uchaguzi huwa zinaandaliwa mwaka wa uchaguzi, lakini kwa kuzingatia unyeti na upekee wa makosa ya ukatili wa kijinsia katika uchaguzi yaliyoongezwa ningependa kujua, je, Serikali haioni umuhimu wa kuandaa kanuni hizi mapema zaidi ili wananchi wapate muda wa kutosha wa kuelimishwa kuhusu kanuni hizi na wale ambao watakuwa wanagombea wajue ni hatua gani za kuchukua pale ambapo wanapitia matukio ya ukatili wa kijinsia katika uchaguzi?
Name
Ummy Hamisi Nderiananga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU (MHE. UMMY H. NDERIANANGA): Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kwanza nimpongeze Mheshimiwa Neema kwa namna ambavyo amelisema suala hili la ukatili wa kijinsia. Pia nimwambie kwamba ushauri wake tumeupokea, tutaendelea kuufanyia kazi. Pia niwatoe wasiwasi Watanzania kwamba tupo vizuri na tutaendelea kuhakikisha kwamba kanuni hizi zinafahamika kwa wananchi wote. Vile vile tutaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali, mashirika yasiyo ya kiserikali, Asasi za Kidini, vyombo vya habari na maeneo tofauti tofauti ili kuweza kutoa elimu.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved