Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Muharami Shabani Mkenge
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bagamoyo
Primary Question
MHE. MUHARAMI S. MKENGE K.n.y. MHE. VINCENT P. MBOGO aliuliza: - Je, lini Serikali itaenda kutatua migogoro ya ardhi ya Kata ya Kala, Ninde na Wampembe - Nkasi Kusini?
Supplementary Question 1
MHE. MUHARAMI S. MKENGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Je, ni lini sasa Serikali itaanzisha mpango maalum wa usuluhishi baina ya mtu na mtu katika masuala ya ardhi ili kupunguza migogoro ya kesi za ardhi Mahakamani?
Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara inaendelea na mikakati mbalimbali ikiwepo eneo moja ambalo tunalifanyia kazi kwa kasi kubwa sana linaloitwa Kliniki ya Ardhi ambapo wale wanaogombana tunawakutanisha, kuwaweka sawa na nia ya kuwapatanisha inakuwepo pale. Hata hivyo, kuhusu masuala ya kupelekana Mahakamani, nadhani watu wengine ni kwa sababu huko mwanzo tulikuwa hatujawa wazi sana juu ya hizi Kliniki na kwa sasa tumeacha mlango wazi na tunaendelea na zoezi hili.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved