Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Festo Richard Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Primary Question
MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. USSI SALUM PONDEZA aliuliza:- Je, Serikali inachukua hatua gani kwa wananchi wanaochukua mafuta baada ya magari ya kubeba mafuta kupata ajali?
Supplementary Question 1
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali. Licha ya hatua hizo ambazo Serikali imekuwa ikichukua, lakini matukio haya yamekuwa yakijirudia mara kwa mara na yamekuwa yakileta madhara makubwa. Ni upi mkakati wa Serikali wa kuchukua hatua kali zaidi kwenye matukio ambayo yanasababishwa inapotokea ajali na watu wanachukua mafuta na baadaye yanaleta madhara makubwa kwenye Taifa letu?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Festo Sanga, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili ni la Watanzania wote. Naomba nitoe kwa jamii nzima ya Watanzania, Viongozi wa Dini pamoja na wazazi na walezi kuhakikisha kwamba, tunaendelea kutoa elimu kwa familia zetu, ili kuhakikisha kwamba, inapotokea ajali si jambo jema kukimbilia kwenda kuiba badala ya kwenda kusaidia. Kwa hiyo, natoa wito kwa jamii nzima tushirikiane kuhakikisha kwamba, jambo hili linakomeshwa mara moja.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia, nakuhakikishia Serikali itaendelea kuchukua hatua kali kwa wale wote ambao wanaiba mafuta haya inapotokea ajali. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved