Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ritta Enespher Kabati
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. JANEJELLY J. NTATE aliuliza:- Je, lini Serikali itaajiri wataalamu wa maabara shule za sekondari, ili kupunguza mzigo kwa walimu wa sayansi kufanya kazi kama wataalamu wa maabara?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba niulize maswali madogo mawili. Kwanza, napongeza majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri. Je, walimu kuandaa vifaa vya maabara hamuoni kama mnapunguza muda wa mwalimu kuandaa masomo yake?
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kwa kuwa Kutunza Maabara ni fani inayotambulika; je, kwa kufanywa na mtu ambaye hana utaalamu hamuwezi kusababisha madhara ya kiutendaji?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba nijibu maswali yake yote mawili kwa pamoja.
Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kuhusu upungufu wa wataalamu wa maabara lakini Serikali inaendelea na jitihada ya kuhakikisha kwamba inaajiri wataalamu hao wa maabara. Kwa wakati huu Serikali inatumia walimu hawa wa sayansi ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaendelea na masomo yao. Sasa sababu ya msingi pia ya kuwatumia walimu wa sayansi ni kwamba walimu wa sayansi na wataalamu wa maabara fani zao zinaingiliana.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo katika mafunzo mwalimu wa sayansi anaweza kufanya kazi ile ambayo mtaalamu wa maabara anaifanya. Kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba jitihada hizi ni za makusudi kabisa ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaendelea kupata elimu na hasa katika masomo ya sayansi. Serikali inaendelea na utaratibu wa kuajiri hawa wataalamu wa maabara na wakishaajiriwa wale walimu wa sayansi wataendelea na kazi zao nao wataalamu wa maabara wataendelea na kazi zao za kitaalamu.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved