Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Tumaini Bryceson Magessa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Primary Question
MHE. TUMAINI B. MAGESSA K.n.y. MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga miundombinu ya umwagiliaji kwenye maeneo ya Wakulima Wadogo wa Chai Tarafa ya Igominyi – Njombe?
Supplementary Question 1
MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza.
Swali la kwanza, ni lini Serikali itaboresha skimu ya umwagiliaji Nyamalulu Jimboni Busanda?
Swali la pili, ni upi mkakati wa Serikali kutumia Ziwa Victoria kuhakikisha kwamba skimu za umwagiliaji zinajengwa na tunaweza kuboresha uzalishaji wa mazao ya chakula?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kuhusu maboresho katika skimu ya Nyamalulu katika Jimbo la Busanda nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba jambo hili lipo katika mpango na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inalifanyia kazi.
Mheshimiwa Spika, mkakati kuhusu Ziwa Victoria tunaendelea nao kwa sababu tuna mkakati wa pamoja kati ya Wizara ya Kilimo, Wizara ya Maji pamoja na Mifugo na Uvuvi ili kuhakikisha maji yale tutakayoyatumia yaweze kuwanufaisha wananchi katika maeneo hayo yote matatu ambayo nimeyataja. Kwa hiyo, lipo katika mipango ya Serikali na litatekelezeka, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved