Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Primary Question

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA (K.n.y. MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM) aliuliza:- Kumekuwepo na ajali nyingi zinazosababisha vifo na majeruhi barabarani, baharini na kwenye maziwa. Je, ni ajali ngapi zimetokea barabarani, baharini na kwenye maziwa kuanzia Januari, 2015 hadi sasa?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri kuhusu masuala ya ajali barabarani. Sasa nina maswali madogo mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza, Tarafa ya Kitunda ambayo iko umbali wa kilometa 180 kutoka Makao Makuu ya Wilaya ya Sikonge ina Kituo cha Polisi kidogo ambacho kina polisi wanne ambao hawatoshi kuhudumia wakazi zaidi ya 80,000 kwenye Tarafa hiyo. Maana kuna majengo chakavu, polisi wenyewe ni wachache na hawana gari hata moja; lini Serikali itawasaidia polisi hao ili wafanye kazi yao vizuri? Hilo la kwanza.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, mwezi Machi, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nyahwa alichinjwa kama kuku na hadi leo wauaji wale hawajakamatwa. Ni lini Serikali itafanya kazi yake kikamilifu ili wauaji hao wakamatwe na kuondoa hofu Kijiji cha Nyahwa? Ahsante sana.

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Kakunda kwamba concern yake ambayo amei-raise hapa tutaifanyia kazi ya kwa maana ya kwamba tutaongeza idadi ya askari katika kituo hicho. Kwa hiyo, nachukua fursa hii kuwaelekeza Jeshi la Polisi wale askari ambao wako depot, tunaotarajia kuwa-deploy karibuni, basi tuangalie uwezekano wa kuwapeleka Sikonge kuongeza ile idadi ya askari waliopungua pale. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pia pale ambapo magari ambayo tunatarajia yataingia wakati wowote, nayo tuone uwezekano wa kufanya hivyo kwa kuzingatia changamoto eneo hilo baada ya kulifanyia utafiti wa kina pamoja na mahitaji ya nchi nzima.

Name

Mboni Mohamed Mhita

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Handeni Vijijini

Primary Question

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA (K.n.y. MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM) aliuliza:- Kumekuwepo na ajali nyingi zinazosababisha vifo na majeruhi barabarani, baharini na kwenye maziwa. Je, ni ajali ngapi zimetokea barabarani, baharini na kwenye maziwa kuanzia Januari, 2015 hadi sasa?

Supplementary Question 2

MHE. MBONI M. MHITA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Naomba nimuulize Mheshimiwa Waziri kwamba Jimbo la Handeni Vijijini ambalo kwa upande mmoja ni barabara kubwa ya Mkata kupitia Korogwe kuja mpaka Misima; ila askari wa Jimbo la Handeni ama Wilaya nzima ya Handeni hawana usafiri wa ku-patrol, jambo ambalo naamini kama wangeweza kuwa na usafiri huo kwa namna moja ama nyingine wangeweza kupunguza idadi ya ajali ambazo zinatokea. Lakini pia, swali langu la piliā€¦
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mboni, swali la nyongeza huwa ni moja.
MHE. MBONI M. MHITA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru.

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, swali hili nalo vilevile tumelichukua. Tutaangalia vilevile utaratibu na hali halisi ilivyo na changamoto ya eneo la Handeni na changamoto za maeneo mengine na idadi ya magari ambayo tutayaingiza kwa awamu inayokuja. Pia tutalipa uzito kwa kutilia maanani changamoto ambazo ametueleza Mheshimiwa Mbunge.

Name

Amina Saleh Athuman Mollel

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA (K.n.y. MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM) aliuliza:- Kumekuwepo na ajali nyingi zinazosababisha vifo na majeruhi barabarani, baharini na kwenye maziwa. Je, ni ajali ngapi zimetokea barabarani, baharini na kwenye maziwa kuanzia Januari, 2015 hadi sasa?

Supplementary Question 3

MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kuniona. Naomba niulize swali la nyongeza.
Kwa kuwa ajali nyingi zinasababishwa na baadhi ya madereva walio wazembe na mfano mzuri ni katika Jiji la Dar es Salaam katika utaratibu mpya ulioanzishwa kwa jitihada za Serikali wa mabasi yaendayo kasi; hadi sasa zaidi ya mabasi 30 yamepata ajali na gharama za matengenezo hayo ni zaidi ya shilingi milioni 90. Je, Serikali inatoa kauli gani kuhakikisha kwamba kama ni sheria, zinawabana madereva wazembe wanaoisababishia Serikali hasara? Ahsante.

Name

George Boniface Simbachawene

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibakwe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba baadhi ya madereva wakiwemo madereva wa pikipiki, bodaboda na magari binafsi na hata magari mengine tu kwa ujumla, bado sharti na sheria inayotaka wasitumie barabara ya mabasi yaendayo kasi inakuwa ngumu sana kwao na hivyo kusababisha ajali.
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niseme kwamba barabara ile ni kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi na siyo vinginevyo. Kwa hiyo, mtumiaji mwingine yeyote anayetumia barabara zile anakuwa amevunja sheria na hivyo, yeye ndiye amegonga yale mabasi na kusababishia hasara.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli takwimu zinaonesha kwamba ajali ni nyingi, na sisi tunasema tutaendelea kusimamia sheria ili kuhakikisha wananchi wanapata elimu, lakini pia watambue kwamba kwa kufanya hivyo wanafanya makosa makubwa na kusababisha hasara. Hawaruhusiwi kutumia barabara za mabasi yaendayo kasi zinazotumika sasa kwa Dar es Salaam.
Kwa hiyo, nawaomba sana wakazi na watumiaji wa barabara Dar es Salaam, kuheshimu barabara za mabasi yaendayo kasi ili kuipunguzia Serikali hasara zinazojitokeza.