Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Stanslaus Shing'oma Mabula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nyamagana
Primary Question
MHE. STANSLAUS S. MABULA aliuliza:- Je, lini Serikali itaipandisha hadhi Barabara ya kutoka Mkolani Darajani – Nyakagwe hadi Busisi kwa kuiondoa TARURA na kuipeleka TANROADS?
Supplementary Question 1
MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Spika, naomba kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa, umuhimu wa barabara hii ambayo inapita Mwasonge – Bulale – Nyakagwe mpaka Mkolani, inaungana moja kwa moja na Daraja la Busisi na tunafahamu liko zaidi ya 90% sasa, linaelekea kukamilika. Serikali haioni umuhimu wa kutengeneza barabara hii ili kupunguza msongamano wa njia kubwa ili hii ndiyo itumike kama njia mbadala?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Nyamagana, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema kwenye jibu la msingi na bahati nzuri binafsi naifahamu hii barabara. Tumeomba wenzetu wa Mkoa wa Mwanza kupitia vikao vyao vya kisheria ambavyo tumevitaja, waweze kuleta maombi katika Wizara ya Ujenzi na wataalamu watakwenda kufanya tathmini. Kama itathibitika kwamba, ina vigezo Wizara haitasita kuipandisha hadhi hiyo barabara na sasa ianze kumilikiwa au kusimamiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved