Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ramadhan Suleiman Ramadhan
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chake Chake
Primary Question
MHE. RAMADHAN SULEIMAN RAMADHAN K.n.y. MHE. TOUFIQ SALIM TURKY aliuliza: - Je, upi mpango wa kuhakikisha viwanda vya kuchinja, kuchana na kusindika nyama vinavyokidhi vigezo vya kusafirisha nje ya nchi vinajengwa?
Supplementary Question 1
MHE. RAMADHAN SULEIMAN RAMADHAN: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, trending inaonesha kwa sasa hoteli, Zanzibar pamoja na Arusha wanaagiza nyama kutoka nje ya nchi, South Africa, Argentina na nchi nyingine. Ni lini Serikali itaweka jitihada za kuhakikisha nyama ya kwetu Tanzania inatumika kwenye maeneo hayo? (Makofi)
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa anachosema Mheshimiwa Mbunge kwamba kuna baadhi ya hoteli ambazo ziko ndani ya nchi zinaagiza nyama kutoka nje ya nchi na hii siyo kwa sababu hatuna viwanda vya Kimataifa. Tuna viwanda vizuri sana vya nyama ndani ya nchi yetu ambavyo vinakidhi vigezo vya Kimataifa na viwanda hivyo vimekuwa vikifanya vizuri ndani ya nchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto tuliyonayo sisi na hili lazima tuambizane ukweli kwamba nyama yetu sisi haina ubora wa kufika nje ya nchi na kupata soko la Kimataifa. Hii ni kwa sababu, sisi tunachokijua ni mfugo kuzaliwa na mfugo kuchinjwa lakini hapa katikati hatufuatilii maendeleo ya mfugo wala hatujui historia yoyote ya mfugo, ikiwa ni pamoja na matibabu ya mfugo. Mfugo huyu anaoga nini hatujui, mfugo anakula nini hatujui, anakunywa tope au maji hatujui, ana chanjo hajachanjwa hatujui. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, wale wenzetu kule nje wanafuatilia hivi vyote na ndiyo maana wanakuwa na kigezo cha kupata soko la Kimataifa. Sasa, nini mkakati wa Serikali? Serikali ndiyo maana tumekuja na mpango wa mwaka huu, lazima mifugo yetu tuichanje kwa lazima nchi nzima ili iweze kupata soko la Kimataifa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tumwombe Mheshimiwa Mbunge pamoja na wadau wengine wa sekta hii ya mifugo kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha kwamba mwaka huu tunaanza zoezi hili la kuchanja mifugo yetu na tupunguze siasa kwenye zoezi hili ili liweze kufanikiwa. Maana yake tumekuwa tukianzisha mipango hii, huko mbele inaingia siasa, mipango inakwama, shughuli zinasitishwa na mambo mengine yanazidi kuharibika.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ili tuweze kupata soko la ndani ya nchi na nje ya nchi ...
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa kwa kifupi.
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: ...lazima tufuate utaratibu wote wa kutibu mifugo yetu ili tuweze kupata soko la ndani ya nchi na nje ya nchi, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved